Jump to content

Kusoma/Wavuti/Ufikivu wa kusoma/Sasisho/2024-04

From mediawiki.org
This page is a translated version of the page Reading/Web/Accessibility for reading/Updates/2024-04 and the translation is 100% complete.

Ufikiaji wa kwanzakwanza wa hali ya giza (mtandao wa rununu, kuingia)

Soma taarifa hii kwa lugha yakoPlease help translate to your language

Habarini nyote, kama ilivyotangazwa mnamo Novemba, timu ya Wavuti katika Shirika la Wikimedia Foundation inashughulikia modi ya giza (wakati fulani pia huitwa hali ya usiku). Sasa, tumezindua kipengele kwa watumiaji walioingia katika akaunti iliyoboreshwa ya simu kwenye miradi yote ya wiki zote kwa madhumuni ya majaribio. Lakini usiogope, kipengele hicho kipya hakisumbui! (Angalia sehemu ya "mapungufu yanayojulikana" hapa chini.) Ni muhimu tushirikiane pamoja nawe kabla hatujakizindua kipengele hiki kwa hadhira pana zaidi. Malengo yetu ya awali kuhusuu usambazaji ni:

  • Kuonesha kile tulichounda mapema sana. Kadiri mnavyoshirikiana nasi mapema, ndivyo sauti zenu zitakavyoonekana katika toleo la mwisho
  • Kupata usaidizi wenu kuhusu kuripoti hitilafu, masuala mbalimbali na maombi
  • Kufanya kazi na wahariri wa kiufundi kurekebisha vigezo na vidude mbalimbali kwa hali ya giza

Nenda kwenye ukurasa wa mradi na Ukurasa wa Maswali yanayoulizwa mara kwa mara ili kuona maelezo zaidi kuhusu misingi ya mradi huu.

Mapungufu yanayojulikana ya toleo lililotangulia

  • Kwa sasa, hali ya giza inapatikana tu kwenye simu ya mkononi, kwa watumiaji walioingia ambao wamechagua hali iliyoboreshwa, kama sehemu ya uhuru wa kuchagua mara mtu atumiapo hali hiyo.
  • Huenda baadhi ya vifaa visifanye kazi vizuri na hali nyeusi na huenda itabidi kuvisasisha.
  • Lengo letu la kwanza ni kufanya hali ya giza ifanye kazi kwenye makala. Kurasa maalum, kurasa za mazungumzo, na nafasi zingine za majina bado hazijasasishwa ili kufanya kazi katika hali nyeusi. Tumezima kwa muda hali nyeusi kwenye baadhi ya kurasa hizi.

Kile ambacho tungependa mfanye (kama jumuiya kwa ujumla)

Ikiwa una maswali - tuulize! Pia, inapofaa, unaweza kujiunga na mjadala kuhusuMapendekezo ya uoanifu wa hali nyeusi kwenye tovuti za wiki za Wikimedia kwenye kurasa zinazoeleza jinsi ya kufafanua rangi katika msimbo. Hivi karibuni, ukurasa huu utasetiwa tayari kwa kutafsiriwa. Tungependa kusisitiza kwamba mapendekezo yanaweza kuzidi kutopokelewa. Kwa sababu hiyo, hatupendekezi kuunda nakala za mapendekezo katika mradi wa wiki yako. Ikifanyika hivyo,wakati fulani, nakala inaweza kuja kuwa tofauti na toleo asilia.

Kile ambacho tungependa mfanye ninyi kama (wahariri wa violezo, wasimamizi wa kiolesura, wahariri wa kiufundi)

Hitilafu nyingi zinapotatuliwa, tutaweza kufanya hali ya giza ipatikane kwa wasomaji kwenye kompyuta za mezani na kwenye simu. Ili hili lifanyike, tunahitaji kufanya kazi pamoja nanyi katika kuripoti na kutatua matatizo.

  1. Ili kuiwasha hali hiyo, tumia tovuti ya simu ya mkononi na uende kwenye sehemu ya |mipangilio ya menyu yako na uchague kuingia katika hali iliyoboreshwa, ikiwa bado hujafanya hivyo. Kisha, seti rangi iwe hali ya giza. (Baadaye, tutaruhusu mapendeleo ya kifaa chenyewe kuweka hali ya giza kiotomatiki).
  2. Baada ya hapo, nenda kwenye nakala tofauti na uone kama utapata changamoto zozote:
    • Ikiwa umegundua tatizo lolote la kigezo na hujui jinsi ya kulitatua
      1. Nenda kwenye ukurasa wa mapendekezo na utafute mfano unaofaa
      2. Ikiwa hakuna mfano unaofaa unaopatikana au huna uhakika wa kurekebisha, wasiliana nasi
    • Ikiwa unataka kurekebisha vigezo vingi katika hali ya giza
      1. Nenda kwenye https://night-mode-checker.wmcloud.org/ na ubainishe vigezo vinavyohitaji kurekebishwa. Zana hii inauwezo wa kuonesha makala 100 bora zilizosomwa zaidi.
      2. Nenda kwenye ukurasa wa mapendekezo na utafute mfano unaofaa
      3. Ikiwa hakuna mfano unaofaa unaopatikana au huna uhakika wa kurekebisha, wasiliana nasi
    • Ikiwa ungependa kutambua matatizo zaidi ya makala 100 bora.
      1. Sakinisha kiendelezi cha kivinjari cha utofautishaji cha rangi cha WCAG (Chrome, Firefox) na utembelee baadhi ya makala. Itumie kutambua matatizo
      2. Nenda kwenye ukurasa wa mapendekezo na utafute mifano inayofaa
      3. Ikiwa hakuna mfano unaofaa unaopatikana au huna uhakika wa kurekebisha, wasiliana nasi
    • Ikiwa una ripoti ya hitilafu ya hali ya giza ambayo haihusiani na violezo
      1. Piga picha ya skrini ya kile unachotazama.
      2. Wasiliana nasi. Ikiwezekana, tafadhali andika toleo la kivinjari chako na toleo la mfumo wa uendeshaji.

Asante. Tunatarajia mtazamo na maoni yako!